Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Sera na Mipango

IDARA YA SERA NA MIPANGO

JUKUMU KUU

 

Kutoa utaalamu na huduma katika uundaji wa sera, utekelezaji; ufuatiliaji na tathmini

Idara ina Sehemu Mbili (2):

 

(i)Sehemu ya Sera na Mipango; na
(ii) Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini.

Idara inaongozwa na; 

          Bi. Joyce Jonathan Momburi

    Mkurugenzi wa Sera na Mipango (DPP)
Email: 
joyce.momburi@mawasiliano.go.tz

WASIFU 

Joyce Jonathan Momburi ni Mkurugenzi katika Idara ya Sera na Mipango, aliyebobea kwenye Sera na Mipango. Kiongozi mwenye uwezo wa kufanya kazi nyingi katika kuratibu, uandaaji wa Sera na Sheria za Sekta pamoja na kupitia upya zilizopo. Amefanikiwa kuratibu shughuli za Sekta, Ufuatiliaji na Tathmini ya programu/miradi mbalimbali, Kutayarisha Sera, miongozo yake;

Amezaliwa na kukulia Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Siha. Joyce alitunukiwa Diploma ya Uchumi katika Maendeleo, Chuo Kikuu cha Bradford, Uingereza; Diploma ya Juu ya Mipango ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tanzania na Baadae kutunukiwa Shahada ya Uzamili wa Sanaa katika Mafunzo ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Bradford, Uingereza.

Joyce, alifanikiwa kufanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kama Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Mkurugenzi Msaidizi (Sera); Wizara ya Fedha, Mipango kama Mchumi na Mchumi Mkuu mtawalia na Afisa Mipango na Udhibiti - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.

Joyce anabaki kuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha kuwa Malengo, Mikakati ya Wizara iliyoainishwa kwenye Mipango Mkakati yanafikiwa kwa manufaa ya Sekta na Nchi kwa ujumla.


MAJUKUMU YA IDARA YA SERA NA MIPANGO

(i) Kuratibu utayarishaji wa sera za Wizara na kufanya tathmini ya utekelezaji wake;

(ii) Kuchambua Sera kutoka sekta zingine na kushauri ipasavyo;

(iii)Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mipango na bajeti za Sekta;

(iv) Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango na bajeti za Sekta na kuandaa ripoti za utendaji;

(v) Kufanya tafiti na tathmini ya Mipango ya Sekta na kutoa msingi wa kufanya maamuzi sahihi juu ya mwelekeo wa baadaye wa Sekta;

(vi) Kuhimiza na kuwezesha utoaji wa huduma kwa Sekta Binafsi katika Sekta;

(vii) Kuratibu maandalizi ya michango ya Sekta kwenye Hotuba ya Bajeti na Ripoti ya Uchumi ya Mwaka;

(viii) Kuwa msimamizi na mratibu wa takwimu za Sekta; na

(ix) Kuhakikisha kuwa mipango na bajeti za Sekta zinajumuishwa katika mchakato wa bajeti ya serikali