Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kitengo cha Fedha

JUKUMU KUU

Kutoa huduma za usimamizi wa fedha na uwekaji hesabu kwa Wizara.


Kitengo cha Fedha na Hesabu kinaongozwa na;

             Bw. Anastasius Pessa (CPA)

               Mhasibu Mkuu (CA).

Barua pepe: anastasius.pessa@mawasiliano.go.tz

WASIFU

Bw. Anastasius C. Pessa anahudumu kama Mhasibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Aidha amewahi kuhudumu kama Mhasibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (2012-2018), Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko (2010-2012), Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Makao Makuu ya Polisi (Jan - Aug 2010), Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala katika Wizara ya Maliasili na Utalii - Chuo cha Taifa cha Utalii(2009) , Mhasibu Mkuu I/Msimamizi wa Programu  katika Wizara ya Sheria na Masuala ya Katiba  - Mpango wa Marekebisho ya Sekta ya Kisheria (2006-2008) , Mhasibu Mkuu DFID - Foundation for Civil Society (2002- 2005), Mhasibu wa Mradi katika Mradi wa CDC - TanWat Sawmill (1997- 2002), Mhasibu wa Mradi katika CDC - Mradi wa Teak wa Kilombero Valley (1995 - 1996), Mhasibu Msaidizi katika Zana Za Kilimo Ltd (1990 – 1995) (Uzoefu wake wa kitaaluma katika fani ya Uhasibu unachukua zaidi ya miaka 28, alioupata katika maeneo mbalimbali aliyohudumu nchini Tanzania.

Bw. Pessa alipata Shahada ya uzamili (MBA)  ya Fedha na Huduma za KiBenki kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe – Kampasi ya Dsm (2005-2007), mwaka 2004 alipata CPA (T) yake kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Diploma ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo – Morogoro (1992 Hadi 1995). Bw. Pessa pia amepata mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Programu ya Usimamizi wa vihatarishi vya Kifedha kutoka Kituo cha Mananga, Ufalme wa Swaziland, Cheti cha Mipango na Udhibiti wa Fedha za Umma kutoka Kituo cha African Rennaissance - Ufalme wa Swaziland, Ununuzi na Usimamizi wa Fedha katika LSRP na Programu ya Kusaidia Marekebisho ya Sekta ya Sheria (LSRP) Kupitia Usimamizi wa Mabadiliko kutoka GTZ- Tanzania, Ulipaji katika Miradi Inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kutoka Benki ya Dunia – Tanzania.

 


 MAJUKUMU YA KITENGO CHA FEDHA NA HESABU;

Ofisi ya Fedha

(i) Kuwasilisha orodha ya vocha Hazina;

(ii) Kukusanya hundi zote kutoka Hazina;

(iii) Fedha taslimu na hundi za benki;

(iv) Kutayarisha ripoti ya kila mwezi;

(v) Kulipa fedha taslimu/hundi kwa wafanyakazi/wateja (Mtoa huduma)

(vi) Hundi za malipo ya vocha;

(vii) Kutunza daftari la fedha,

(viii) Kutunza kumbukumbu za masurufu yote yaliyotolewa; na

(ix) Kutayarisha na kutekeleza malipo yote

Mapato

(i) Kukusanya mapato yote;

(ii) Kusimamia mapato kwa mujibu wa kanuni na miongozo;

(iii) Kukusanya kodi ya mwaka, ada za maombi na ada nyinginezo; na

(iv) Kufanya usuluhishi wa Benki.

Bajeti

(i) Kufuatilia mgao na matumizi; na

(ii) Kuandaa Hesabu za Mwisho na taarifa nyingine za fedha.

Kuhakiki na kukagua  nyaraka na vocha zilizoidhinishwa kabla ya malipo

(i) Kuthibitisha nyaraka sahihi za kusaidia vocha ikiwa ni pamoja na idhini kulingana na kanuni;

(ii) Kuchunguza nyaraka za mwisho ili kuhakikisha uzingatiaji wa sheria husika, kanuni, waraka n.k; na

(iii) Kujibu hoja zote za Ukaguzi zilizoulizwa katika mwaka wa fedha uliopita.