Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Idara ya Mawasiliano

LENGO;

Kutoa utaalamu wa Sera, Mikakati na Miongozo ya Kitaifa ya maendeleo ya mawasiliano.

Idara ina Sehemu tatu (3): (i)Sehemu ya Uwekezaji wa Mawasiliano;

(ii) Sehemu ya Huduma za Mawasiliano na Utangazaji; na (iii) Sehemu ya Huduma za Posta.

Idara inaongozwa na;

 

    

Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano (DC)

Email: 

 


MAJUKUMU YA IDARA YA MAWASILIANO

(i) Kuanzisha, kutunga na kupitia sera za Mawasiliano, Mikakati na miongozo ya maendeleo ya sekta;
(ii)Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera, mikakati na miongozo ya Mawasiliano,
(iii) Kuratibu utangazaji na matumizi ya bidhaa na huduma za Mawasiliano kwa maendeleo ya Taifa;
(iv) Kuratibu Huduma za Taifa za Mawasiliano ili kuwezesha sekta nyingine za uchumi;
(v) Kuweka mazingira mazuri ya kukuza uwekezaji katika sekta ya mawasiliano;
(vi) Kuimarisha upatikanaji na uwezo wa kumudu bidhaa na huduma za mawasiliano kwa umma;
(vii) Kukuza na kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Huduma za Mawasiliano kwa Wote;
(viii) Kukuza na kuwezesha maendeleo ya taasisi za huduma za mawasiliano;
(ix) Kusimamia mawasiliano ya Kikanda na Kimataifa katika dhamira ya kuharakisha ubia;
(x) Kuweka mifumo ifaayo inayokuza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika matumizi na usimamizi wa huduma za Mawasiliano; na
 (xi) Kukuza ushindani katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.