Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA

KITENGO CHA MIUNDOMBINU YA TEHAMA

LENGO

Kutoa utaalamu wa Miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano ili kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi


Kitengo kinaongozwa na;

                    Mhandisi Leo Magomba

               Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu (DICTI)

WASIFU

Mhandisi Leo Magomba ni Mhandisi Mtaalamu aliyesajiliwa na bodi ya Wahandisi katika tasnia ya uhandisi wa Kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).  Mhandisi Leo Magomba ana uzoefu wa kiuhandisi wa zaidi ya miaka kumi na tano (15) katika tasnia ya TEHAMA. Ni mhandisi mwenye uzoefu mpana na maarifa ya kina katika Ukuzaji na Uongozi katika TEHAMA na jamii ya maarifa pamoja na kubuni, kupanga, utekelezaji, uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya TEHAMA/Mawasiliano na Usimamizi wa Miradi. Amehusika kuleta mawazo na kutoa masuluhisho kiufundi ya kidijitali ambayo yameleta mabadiliko chanya kwenye uchumi wa kidijitali na maendeleo ya jamii maarifa.

Mhandisi Leo magomba amehusika kwenye miradi mbalimbali ya Miundombinu ya TEHAMA kwa zaidi ya miaka 15 ikiwemo Ujenzi wa Mkongo wa Taifa (NICTBB), Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), Miundombinu ya Kiitifaki ya Data (IP/MPLS), Ujenzi wa Mindombinu ya Mtandao Serikali (GOVNET), Ujenzi wa Miundombinu Mikuu (Core and Backbone Networks), Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ya mijini (Metro), Miundombinu ya kuunganisha wateja (Last Mile Connectivity) na Ujenzi wa Mindombinu ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya 2G/3G/4G.

Amekuwa kiongozi na msimamizi wa masuala ya sekta ya TEHAMA kwa zaidi ya miaka 10.


MAJUKUMU YA KITENGO

(i) Kuandaa sera, sheria, kanuni, miongozo na viwango kuhusu maendeleo ya miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano.

(ii) Kuunda Mpango wa kitaifa wa maendeleo ya miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano na kufuatilia utekelezaji wake.

(iii) Kuwezesha uanzishwaji wa mazingira mazuri ya ushirikiano na ushirikishwaji katika maendeleo ya miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano miongoni mwa wadau katika ngazi zote zikiwemo sekta za umma na binafsi.

(iv) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa miradi ya kitaifa ya miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano ikijumuisha, vituo vya kuhifadhi data (datacenter), NICTBB (National ICT Broadband Backbone)  na PKI n.k inayotekelezwa na Taasisi husika kwa kuzingatia sera ya Taifa ya TEHAMA.

(v) Kukuza ushirikiano na sekta nyingine zinazotekeleza miradi ya kitaifa inayonuia kupeleka miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano (Kama vile usambazaji wa Nishati, Reli, Mafuta, Gesi n.k)

(vi) Kuhakikisha uwepo wa mfumo shirikishi wa kuongoza uwekaji wa miundombinu ya TEHAMA na Mawasiliano na ushiriki wa pamoja wa ujenzi wa miundombinu hiyo.

(vii) Kukuza miundombinu iliyo tayari ya kielektroniki iliyojengwa nchini kote ambayo inasaidia utoaji wa huduma za TEHAMA; na

(viii) kuhakikisha miundombinu salama na ya kuaminika ya TEHAMA inaendelezwa kote nchini.