Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Miradi Iliyo Kamilika

 

ORODHA YA MIRADI ILIYOKAMILIKA

Na.

JINA LA MRADI

MUDA WA UTEKELEZAJI WA MRADI

TAREHE YA KUANZA KWA MRADI

TAREHE YA KUKAMILIKA KWA MRADI

MAENEO YA MRADI/ WAFAIDIKA NA MRADI

 

MFADHILI

1.

Mradi wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya I.

Miezi 18

2009

2010

Katika mradi huu wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya I jumla ya kilomita 2,280 zilijengwa. Aidha, katika Awamu hii Mkongo wa Taifa uliunganishwa pia na Mikongo ya Baharini ya SEACOM na EASSy.

 

 

 

 

 

 

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia mkopo wenye Masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya China

2.

Mradi wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya II.

Miezi 18

2010

2012

Katika mradi huu wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya II jumla ya  kilomita 3,168 zilijengwa.

3.

Mradi wa Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Awamu ya III.

Miezi 18

2014

2016

Katika Ujenzi wa Mkongo wa Taifa Awamu ya III jumla ya Kilomita 100 zilijengwa Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Pemba. Awamu hii ilijumuisha ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Data (National Internet Data Centre) Dar es Salaam, ufungaji wa mitambo kwa ajili ya mtandao wa miundombinu ya itifaki [Internet Protocol-Multilayer Label Switching (IP-MPLS) Network], Upanuzi wa Mkongo na kuunganisha Zanzibar kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Aidha, hadi sasa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeunganisha Makao Makuu ya mikoa 25 ya Tanzania Bara ambapo katika Mikoa hiyo Mkongo wa Taifa umefika kwenye Wilaya 42 kati 139 na una urefu wa Kilomita 7,910.

4.

Mradi wa kuunganisha Ofisi za Halmashauri   kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Miezi 10

Juni 2018

Aprili 2019

Mradi huu umehusisha kuunganisha kwenye mawasiliano Halmashauri 10 zifuatazo; Katesh, Uvinza, Wanging’ombe, Urambo, Kaliua, Mbulu, Monduli, Sikonge, Simanjiro na Kiteto.

 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

5.

Mradi wa kuunganisha Ofisi mbalimbali za Serikali pamoja na Halmashauri zipatazo kwenye Mkongo wa Taifa wa mawasiliano

Miezi 12

Agosti 2019

Agosti 2020

Mradi huu umehusisha kuunganisha kwenye mawasiliano jumla ya Ofisi 18 za Serikali pamoja na Halmashauri zilizopo katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Kagera, Mbeya, Arusha, Mtwara, Lindi, Geita, Shinyanga, Tanga na Pwani. Ofisi zilizounganishwa ni; Igoma Kituo cha Afya, Misungwi Kituo cha Afya, Kisesa Kituo cha Afya, Maktaba ya Dodoma, Kituo cha Afya Makole, Hospitali ya Mirembe, Halmashauri ya Kondoa, Halmashauri ya Ileje, Ngarenaro Kituo cha Afya, Kaloleni Kituo cha Afya, Halmashauri ya Mtwara, Halmashauri ya Lindi, Nyangao Hospitali, Halmashauri ya Geita, Halmashauri ya Kishapu, Maramba Kituo cha Afya-Mkinga, Ngamiani Kituo cha Afya na Halmashauri ya Mafia.

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

 

6.

Mradi wa kuunganisha Ofisi mbalimbali za Serikali na Halmashauri kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Miezi 15

Mei  2019

Agosti 2020

Mradi huu ulihusisha kuunganisha ofisi 23 za Serikali pamoja na Halmashauri zilizopo kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Geita, Arusha, Morogoro, Katavi, Rukwa, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Geita, kuunganishwa kwa mawasiliano kwa njia ya mkongo. Na pia mradi huu ulihusisha ukarabati wa Njia ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ya Arusha-Namanga. Ofisi kutokana na mradi huu ni zifuatazo; Posta Siha, Siha Hospitali ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Siha, Mkuu wa Wilaya-Siha, Mkurugenzi Mtendaji-Bukombe, Bukombe Hospitali, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Ngorongoro, Mkuu wa Wilaya-Ngorongoro, Mahakama-Ngorongoro, Magereza-Ngorongoro, Polisi-Ngorongoro,  Ngorongoro Hospitali, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Mvuha, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Nsimbo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya-Mlele, Ofisi ya Rais-Mlele, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya-Kalambo, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya-Buhigwe, Buhigwe Hospitali, ITETE DDH, Mkuu wa Wilaya-Busekelo, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya-Buchosa, na Buchosa Hospitali.

 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

 

7.

Mradi wa kuwezesha Miundombinu ya Mawasiliano ya Kikanda Tanzania- Tanzania Communications Infrastructure and eGovernment Project (Regional Communications Infrastructure Program – RCIP Tanzania Project)

 

Miezi 84

                         

Januari 2010

 

Desemba 2017

Utekelezaji wa mradi huu umekuwa na matokeo chanya na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Baadhi ya Matokeo hayo ni kama ifuatavyo;

 1. Serikali iliweza kutunga sheria za kusimamia matumizi ya mifumo na mitandao ambazo ni “Cyber Crime Act, 2015” pamoja na” Electronic Transaction Act, 2015”. Pia rasimu ya sheria ya utunzaji wa taarifa binafsi (Personal Data Protection Bill) na mkakati wa usalama wa mtandao “Cyber Security Strategy vimeandaliwa;    
 2. Serikali ilikamilisha utengenezaji wa miongozo ya viwango vya serikali mtandao (eGovernment Standards and Guidelines) kwa ajili ya kuhakikisha mifumo inayowekwa na taasisi za serikali inakuwa salama, yenye viwango na inayoweza kubadilishana taarifa; 
 3. Serikali ilinunua na kulipia mkondo wa mawasiliano wa kimataifa “international Internet bandwidth” ya ukubwa wa 2.1Gbps kwa kipindi cha miaka kumi (10) kuanzia mwaka 2012 hadi 2022 kwa ajili ya matumizi ya serikali na taasisi zake pamoja na vyuo vya elimu ya juu; 
 4. Serikali imeweza kutanua wigo wa matumizi ya TEHAMA hadi maeneo ya vijijini, baada ya kuzipatia ruzuku (subsidy) Kampuni za simu, ili ziweze kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo ya mazingira magumu kufikika;
 5. Serikali imejenga Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali- GovNet ambao umeunganisha Taasisi za Serikali 189 zikijumuisha Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Mamlaka ya Serikali za Mitaa ziliunganishwa kwenye mtandao mmoja wa serikali (Independent Government Communications Network) hadi kufikia Disemba, 2017; na
 6. Serikali imeweza kujenga Kituo cha data za Serikali (Government Data Centre) ambacho kinafanya kazi sambamba na Kituo cha Kitaifa cha Data (National Internet Data Centre);
 7. Shule za Sekondari zipatazo 129 zilipatiwa vifaa vya TEHAMA;
 8. Wizara kupitia mradi wa RCIP ilikamilisha ufungaji wa mitambo ya video conference 17 katika Mikoa na Ofisi za Serikali na Zanzibar na hivyo kufanya jumla ya video conference kuwa 43;
 9. Kupitia mradi wa RCIP, Wizara imekamilisha kazi ya kuandaa upembuzi yakinifu (Feasibility Study) wa National Public Key Infrastructure (NPKI);
 10. Jumla ya kata 286 (yenye jumla ya vijiji 1,279) na kati ya kata 347 (yenye Jumla ya Vijiji 1393) vilifikishiwa huduma ya mawasiliano nchini na hivyo kufanya huduma za mawasiliano kupatikana kwa asilimia 94 nchini;
 11. Kukamilika kwa Mfumo wa Usajili wa Biashara kwa Mtandao ambao umekuwa ndiyo dirisha kuu la kutolea huduma na taarifa za biashara nchini;
 12. Kukamilika na kuanza kutumika kwa Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo tangu Disemba 2017;
 13. Mfumo wa tiba mtandao ulikamilika na kufungwa katika vituo nane (8) vilivyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili; Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Morogoro na Lindi; Hospitali za Wilaya za Kilosa, Turiani, Mafia, Nyangao na Nachingwea;
 14. Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeweza kutengeneza mfumo wa e-Office ambao unatumiwa na Taasisi za Serikali katika kurahisisha utendajikazi wa kila siku;
 15. Kukamilika na kuanza kutumika kwa Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Mtandao (Tanzania National e-Procurement System-TANePS);
 16. Utengenezaji wa Mfumo wa Nyaraka Mtandao (Trusted Digital Records Management and Preservation System)

umekamilika na unaendelea kutumika na kuweza kusaidia upatikanaji wa haraka wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Serikali na pia kuongeza ufanisi wa uhifadhi na upatikanaji (kwa njia ya kielectroniki) wa kumbukumbu hizo kwa taasisi za serikali, watafiti na wananchi kwa ujumla;

 1. Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao iliweza kuanzisha “Mobile Platform” kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kupitia simu za mkononi; na
 2. Programu ya mafunzo ya RCIP ndani na nje ya nchi ilitekelezwa. Watumishi zaidi ya 2,066 walihudhuria mafunzo, warsha, kongamano na kozi fupi yaliyohusiana na TEHAMA.

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mkopo kutoka Benki ya Dunia