Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara ya kukagua mtambo wa uchapaji kibiashara (Hybrid Web Offset) wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika eneo ulipohifadhiwa Tazara, jijini Dar es Salaam, leo Machi 19, 2023.
Naibu Waziri wa HMTH, Mhe. Mhandisi Kundo A. Mathew akimpongeza mshindi wa tuzo za WSIS kutoka taasisi ya Apps and Girls Tanzania Bi. Carolyne Ekyarisiima, katika kipengele cha ajira kwa njia ya mtandao kupitia mradi wao wa ujasiriamali kwa wasichana kupitia TEHAMA.
Naibu Waziri wa HMTH, Mheshimiwa Kundo A. Mathew na NKM- WHMTH Bw. Selestine Kakele wakifurahia za tuzo ya WSIS katika kipengele cha ajira kwa njia ya mtandao iliyochuliwa na taasisi ya Apps and Girls Tanzania kupitia mradi wao wa ujasiriamali kwa wasichana kupitia TEHAMA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Selestine Gervas Kakele ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Kimataifa la Jamii ya Habari na Mawasiliano (WSIS Forum 2023) linalofanyika Geneva, Uswisi tarehe 13-17 Machi 2023
Kaimu KM na Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi cha Wizara ya WHMTH, Bw. Armon MackAchayo akiwa kwenye Picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu Bi. Salome Kessy (kulia) aliyehamia na Bi. Teddy Njau (Kushoto ) aliyehamishiwa Wizara ya Maji.
Waziri wa HMTH, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akikabidhi Tuzo za Kutambuliwa Ushiriki wa Wanawake katika TEHAMA wakati wa Kongamano la Wanawake wa Tanzania Katika TEHAMA leo Machi 07, 2023 , jijini Dar es Salaam.
Mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo wenye teknolojia ya 2G na 3G uliojengwa kwa ruzuku kutoka UCSAF katika kata ya Noondoto wilaya ya Longido mkoani Arusha
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza na wanafunzi kuhusu ujio wa kompyuta ni namna gani itawasidia katika masomo yao msomera wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga leo machi 1 2023
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Nape Nnauye (Mb) na Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando (kushoto) wakikagua maabara za kompyuta katika shule ya msomera wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga leo machi 1 2023
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya mawasiliano na TEHAMA katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw.Mohammed Khamis Abdulla akimkabidhi zawadi yenye ujumbe wa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw.Selestine Gervas Kakele leo februari 28,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa WHMTH Bw.Mohammed Khamis Abdulla akimkabidhi zawadi yenye ujumbe wa shukrani aliyekuwa KM-WHMTH na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, na Uratibu Dkt. Jim Yonazi kwa niaba ya Mhe.Nape Nnauye, Waziri wa HMTH, februari 28, 2023 jijini Dodoma
KM wa WHMTH, Bw. Mohammed Khamis Abdulla (Kulia) akimkaribisha NKM wa WHMTH, Bw. Selestine Gervas Kakele katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Dodoma, Februari 27, 2023
KM wa WHMTH, Bw. Mohammed Khamis Abdulla (Kulia) akipokelewa na Menejimenti ya Wizara katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Dodoma, Februari 27, 2023 wa pili kushoto ni NKM wa WHMTH, Bw. Selestine Gervas Kakele
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo jijini Arusha.
Muonekano wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) linaloendelea kujengwa jijini Arusha.
Waziri wa HMTH Mhe. Nape Moses Nnauye, Februari 15. 2023 Amefanya Ziara katika kituo cha televisheni cha Chanel Ten Jijini Dar es Salaam, Katika ziara hiyo amepongeza kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari katika kutangaza mambo yanayofanywa na Serikali ya Tanzania.
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye Alipofanya ziara katika kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Katika ziara hiyo iliyofanyika Leo Februari 15 2023 Waziri Nape ameeleza nia ya Serikali ya kuboresha sekta ya habari nchini katika nyanja mbalimbali.
Wizara WHMTH yasaini makubaliano ya kuboresha bunifu na kampuni changa nchini
Katibu Mkuu wa WHMTH, Dkt. Jim Yonazi ameongoza Watumishi wa Wizara hiyo katika zoezi la upandaji miti katika jengo jipya la Wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma Februari 9,2023
Waziri wa HMTH, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha Naibu Waziri wa Biashara za Kimataifa wa Marekani Bi. Maria Lago, leo Februari 7, 2023 jijini Dodoma .
Naibu Waziri wa HMTH, Mhe. Mhandisi kundo Mathew (Mb) akikabidhi zawadi ya kipekee kwa msichana aliyefanya vizuri kuliko wasichana wote, Magreth Haule katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni yaliyofanyika Februari 07, 2023 katika ukumbi wa PSSSF, jijini Dodoma
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akiagana na Waziri wa Mambo ya Uchumi wa Finland Mhe. Mika Lintillå baada ya mazungumzo baina ya Wizara na ujumbe kutoka Finland leo Januari 31, 2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu WHMTH, Dkt. Jim Yonazi akiagana na Waziri wa Mambo ya Uchumi wa Finland Mhe. Mika Lintillå baada ya mazungumzo baina ya Wizara na ujumbe kutoka Finland leo Januari 31, 2023 jijini Dodoma.
Waziri wa HMTH, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza na ujumbe wa Serikali ya Finland ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Uchumi wa Finland Mhe. Mika Lintillå (kushoto) leo Januari 31, 2023 jijini Dodoma. Menejimenti ya WHMTH ikiongozwa na Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) ilishiriki kikao hicho.
Kichwa | Tarehe | Pakua |
---|---|---|
KANUNI ZA TARATIBU ZA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO DHIDI YA UKIUKWAJI WA MISINGI YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI ZA MWAKA 2022 | 2023-02-14 | Pakua |
MUSWADA WA SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI | 2022-10-09 | Pakua |
ELIMU YA USALAMA MTANDAO | 2022-10-07 | Pakua |
MWEZI WA UHAMASISHAJI NA UELIMISHAJI WA MATUMIZI SALAMA YA MTANDAO | 2022-10-07 | Pakua |
CYBERCRIME ACT 2015 | 2022-10-07 | Pakua |