Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Maelezo Kuhusu Wizara

 

KUANZISHWA KWA WIZARA NA MAMLAKA  YAKE 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alianzisha Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Notisi ya Serikali Na. 619A na 619B ya tarehe 30 Agosti, 2023 kama ilivyofanyiwa marekebisho kwa Notisi ya Serikali Na. 35 na 36 ya tarehe 17 Januari, 2025. Wizara hii ilipewa mamlaka ya kuandaa Sera za Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (TEHAMA), Posta na Mawasiliano ya Simu pamoja na utekelezaji wake; Utafiti, Maendeleo na Ubunifu katika TEHAMA; Maendeleo ya Wataalamu wa TEHAMA; Uanzishaji na Usimamizi wa Mifumo ya Anwani za Posta; Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Ulinzi na Usalama wa TEHAMA; Uboreshaji wa Utendaji na Maendeleo ya Rasilimali Watu chini ya Wizara; pamoja na Idara zilizoko nje ya Wizara, Mashirika ya Umma; Wakala na Miradi iliyo chini ya Wizara hii.

MAADILI YETU

Uadilifu: Tunawatendea wateja wetu na wadau wengine kwa haki na kwa adabu. Tunazingatia maadili wakati wa kutekeleza majukumu yetu na kudumisha usiri.

Uwazi: Tunasambaza taarifa muhimu kuhusu huduma na bidhaa zetu kwa umma.

Kazi ya pamoja: Tunatumia utaalamu mbalimbali katika kufikia malengo yetu.

Taaluma/Uweledi: Tunatumia ustadi wa hali ya juu na umahiri katika kutekeleza majukumu yetu.

Ubunifu: Tunatengeneza mbinu na mawazo mapya ambayo husababisha matokeo chanya katika sekta hii.

Uwajibikaji: Tunawajibika kwa vitendo na maamuzi tunayofanya wakati wa kutekeleza majukumu yetu.