Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini

KITENGO CHA UFUATILIAJI NA TATHMINI

JUKUMU KUU

Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera, Mpango Mkakati wa Muda wa Kati (MTEF), mipango ya mwaka, bajeti, programu na miradi iliyo chini ya Wizara


Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kinaongozwa na;

Bw. Elisa D. Mbise

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini.

Email: elisa.mbise@mawasiliano.go.tz

WASIFU

Bwana Mbise Kitaaluma ni Mchumi. Amewahi kuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na baadae akaendelea na nafasi hiyo kwenye Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (2018-2023). Alishakuwa Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Bajeti) kwenye Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) kuanzia 2006 -2018.

Bwana Mbise alifanya kazi Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama Mkurugenzi Msaidizi na Mkuu wa Sehemu ya Mipango 2007-2016, Katibu Msaidizi wa Bunge ambapo alikuwa Katibu wa Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo na Ardhi na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama 2000-2007. Aidha, Bwana Mbise aliwahi kuwa Mratibu wa Kamati ya Kudumu Bunge ya Bajeti baada ya kushiriki katika uanzishwaji wa Kamati hiyo. Katika kipindi hicho Bwana Mbise alikuwa Mratibu wa Miradi ya Kujengea Uwezo Wabunge ukiwemo Deepening Democracy in Tanzania Programme na Legislatures Support Project.

Bwana Mbise amekuwa mjumbe kwenye Bodi mbalimbali ikiwemo Bodi ya Taifa ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha za Kivita, Bodi ya Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi, Ofisi ya Bunge, Mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), na Mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, wadhifa anaondelea nao hadi hivi sasa.

Bwana Mbise ana Shahada ya Uzamili (MBA) katika usimamizi wa Fedha aliyopata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2005), Shahada ya Kwanza katika Uchumi (BA Economics – Hons) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995).

Aidha, Bwana Mbise amepata mafunzo ya  muda mfupi kama ifuatavyo:=

Certificate in Budget and Financial Management, Project Appraisal and Risk management – DukeUniversity, Sanford School of Public Policy, NC USA, 2006, 22008 ii. Certificate in Public Policy Management, Strathmore University, Nairobi Kenya, 2013 iii. Public Administration and Civil Service management, Galilee International Management Institute, Israel 2014 iv. Executive Training on Good Governance, New Zealand, Australia and Thailand, 2015 v. Twelfth Leaders’ Capstone Course – National Defense College, Dar Es Salaam. 


MAJUKUMU YA KITENGO

(i) Kufuatilia na kutathmini Maeneo Muhimu ya Kitaifa ya Matokeo (NKRAs) kwa Wizara;

(ii) Kufanya tathmini ya athari za muda mrefu kwenye mipango, programu na miradi iliyo chini ya Wizara;

(iii) Kuandaa na Kutekeleza Muundo na Mfumo wa U&T wa Wizara;

(iv) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya tathmini;

(v) Kutayarisha Taarifa za mara kwa mara za U&T kuhusu NKRAs chini ya Wizara;

(vi) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala na maagizo ya Serikali;

(vii) Kufuatilia na kutathmini utendaji wa muda na tathmini za mara kwa mara za Wizara;

(ix) Kufuatilia utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara;

(x) Kuratibu mapitio ya utendaji Kitaasisi/ Mfumo wa Taarifa za Utendaji wa Taasisi za Umma (PIPMIS); na

(xi) Kuwa mwangalizi wa Takwimu za Wizara.