Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa TEHAMA

LENGO
Kuwa na mazingira salama ya kusaidia matumizi ya mawasiliano, Bidhaa na Huduma za ICT.

Kitengo kinaongozwa na;

Bw. Mussa Patrick Chiwelenje

Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa TEHAMA (DISS)

Barua pepe; mussa.chiwelenje@mawasiliano.go.tz

WASIFU WA BW.MUSSA CHIWELENJE.

Bw. Mussa Patrick Chiwelenje ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Aidha, Bw. Chiwelenje ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika tasnia ya TEHAMA.

Kabla ya wadhifa huu, Bw. Chiwelenje aliwahi kuhudumu kama Katibu wa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari; Afisa Bunge wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Afisa TEHAMA katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Kielimu, Bw. Chiwelenje alipata Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Habari na Mawasiliano (Master’s Degree in Information and Communication Engineering) kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Huazhong, Wuhan - China.

Aidha, Bw. Chiwelenje amepitia mafunzo ya masuala ya Usalama Mtandao kutoka katika Taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Infotronix Technologies (India), Unique Academy (Tanzania) na CYBERGEN (Tanzania).


MAJUKUMU YA KITENGO CHA USALAMA WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI

(i) Kuandaa sera, sheria, mkakati, miongozo na kanuni zinazohusiana na Usalama na Usalama wa mawasiliano na teknolojia ya habari;

(ii) Kuanzisha utaratibu sahihi wa kuwezesha utekelezaji wa usimamizi wa usalama wa mawasiliano nchini;

(iii) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera za usalama wa mawasiliano na teknolojia ya habari,

(iv) Kuweka mazingira sahihi ya kuwezesha utekelezaji wa hatua za kuzuia uhalifu wa kimtandao nchini;

(v) Kuratibu maendeleo ya mikakati na mpango wa kukuza usalama wa vifaa vya teknolojia ya mawasiliano.

(vi) Kuratibu maendeleo ya mikakati na mpango wa kukuza mwendelezo wa Biashara na uzuiaji wa majanga mbalimbali ya usalama wa mawasiliano;

(vii) Kukuza mipango ya teknolojia ya mawasiliano; Na

(viii) Kufanya ukaguzi wa mifumo ya Tehama ili kuhakikisha kuwa inaendana na mahitaji ya usalama wa mawasiliano.