Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

ZIARA YA KIKAZI MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA MINARA 42 ZANZIBAR


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amefanya ziara ya kukagua minara 42 itokanayo na mradi wa Rural Telecommunication Border & Special Zone Phase 7 (BSZPH7) ilyojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na kampuni ya  Tigo-Zantel tarehe 29 Agosti, 2022, Zanzibar.
 
Kupitia ziara hiyo, Bw. Mohammed Abdulla amezipongeza UCSAF na kampuni ya Tigo-Zantel kwa utekelezaji wa mradi huo kwa ufanisi mkubwa na kupelekea kupunguza tatizo kubwa la huduma za mawasiliano katika maeneo mbalimbali ya unguja vijijini.
 
Sambamba na hilo Bw. Mohammed Abdulla pia amewataka kampuni ya Tigo-Zantel kuweka nguvu kubwa katika kuilinda miundombinu hiyo kwani imegharimu fedha nyingi mpaka kukamilika kwake.
 
Mpaka sasa jumla ya minara 40 kati ya 42 imekwisha jengwa na kuwashwa. Minara miwili iliyobaki ni ya shehia za Kombeni (Kitongoji cha Kisakasaka) na Matale (Kitongoji cha Mfikiwa) ambapo utekelezwaji wake utaanza hivi karibuni.