Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WIZARA YAPANDA MITI KATIKA JENGO LA OFISI YA WIZARA LILILOPO MJI WA SERIKALI MTUMBA


Leo Februari 09, 2023 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi ameongoza Watumishi wa Wizara hiyo katika zoezi la upandaji miti katika jengo jipya la wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bi. Teddy Njau akipanda mti aina ya Mtimaji (Mdodoma) katika jengo jipya la wizara hiyo lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2023.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakipanda mti aina ya Mtimaji (Mdodoma) katika jengo jipya la wizara hiyo lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2023.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya zoezi la upandaji miti katika jengo jipya la wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2023.