Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WIZARA YA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI YATOA ELIMU KWA WANANCHI KUPITIA BANDA LA MAONESHO


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

Banda la Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park, Dodoma, limetembelewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa lengo la kujionea na kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi.

 

Akizungumza katika banda hilo, Afisa Biashara seksheni ya Mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA) Bi. Winifrida Silayo amesema kuwa moja ya huduma muhimu zinazotolewa ni elimu kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi, ambapo wananchi wanaelekezwa namna ya kutambua na kupata anwani zao za makazi pamoja na barua za utambulisho kwa urahisi.

 

Aidha, kwa upande wa mifumo ya kidijitali, Bi. Winifrida Silayo amesema kuwa mifumo inayosimamiwa na Wizara imechangia kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma, hivyo kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma.

 

Bi. Silayo ameongeza kuwa wananchi wanaotembelea banda la Wizara hupatiwa elimu kuhusu mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayosimamiwa na Wizara, ikiwemo Mfumo wa Anwani za Makazi, ili kuwawezesha kunufaika na huduma za kidijitali zinazotolewa na Serikali.

Maadhimisho hayo yanaendelea chini ya kaulimbiu isemayo "Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu."