Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WIZARA YA HABARI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KWA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU


Na Juma Wange, WHMTH, Dodoma

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 pamoja na makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.


Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Moshi Kakoso (Mb) na kuhudhuriwa na Wajumbe mbalimbali wa Kamati hiyo.

Kwa upande wa Wizara, Waziri wa Habari, MawasilianonaTeknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) aliongoza viongozi mbalimbali kati yao ni Naibu Waziri, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Bw. Selestine Gervas Kakele, Wakurugenzi wa Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.