Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WIZARA YA HABARI KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KATIKA TEHAMA


Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla amekutana na kufanya mazungumzo na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kikao kilichofanyika tarehe 01 Oktoba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

Bw. Abdulla ameongoza kikao hiko akiwa na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambao walijadili maeneo ya ushirikiano katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hususan ushiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika uanzishwaji wa program za Chuo Mahiri cha TEHAMA (DTI), Teknolojia ya Satelaiti pamoja na vituo vya Ubunifu na Atamizi (Softcenters and incubators) katika TEHAMA nchini.

Katika kikao hicho, wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliongozwa na Naibu Makamu Kansela (Utafiti) Professa Bernadetha Killian.