Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI SILAA AKUTANA NA UONGOZI WA VODACOM GROUP


Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), amekutana na kuzungumza na uongozi wa Kampuni ya Vodacom Group, leo tarehe 01 Oktoba, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Kampuni ya Vodacom Group iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Group, Bw. Sakumzi Macozoma, pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Kampuni ya Vodacom Group na Uongozi wa Vodacom Tanzania.

Waziri Silaa alishiriki mazungumzo hayo akiwa na wataalamu wa huduma za Mawasiliano na Miundombinu ya TEHAMA kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari waliojadili  masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini.