Habari
WAZIRI SILAA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA MULTICHOICE TANZANIA
Leo Novemba Mosi, 2024, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Keabetswe Modimoeng, Afisa Mkuu wa Uhusiano na Masuala ya Udhibiti wa Makampuni ya MultiChoice kuhusiana na mashirikiano katika Sekta ya Utangazaji
Katika kikao hicho Dkt. Keabetswe aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji Maltchoice Tanzania, Jacqueline Woiso, Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana na Mkuu wa Masuala ya Udhibiti-MultiChoice Tanzania Astrid Mapunda.