Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI SILAA AELEKEZA MAMBO 11 UZINDUZI BODI YA SHIRIKA LA POSTA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), leo tarehe 18 Novemba 2024, amewaelekeza mambo kumi na moja (11) Bodi ya Shirika la Posta wakati wa hafla ya kuzindua bodi hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

## Maelekezo ya Waziri Silaa:

 1.⁠ ⁠*Maboresho ya Sera:*  
   Waziri Silaa ameitaka Bodi kushirikiana na Wizara kuhakikisha Sera ya Posta ya mwaka 2003 inafanyiwa maboresho, na maboresho hayo yaakisiwe kwenye Sheria ya Shirika ya mwaka 1993.

 2.⁠ ⁠*Boresha Utendaji:*  
   Shirika linapaswa kuboresha utendaji kazi kwa kuhamasisha matumizi ya TEHAMA na kuongeza ubunifu ili kuendana na mahitaji ya soko.

 3.⁠ ⁠*Utekelezaji wa Sheria:*  
   Shirika lihakikishe linatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria iliyopo na kujiimarisha ili kuondoa matamanio ambayo yanaweza yasifikishe Shirika kunakopaswa.

 4.⁠ ⁠*Mradi wa Maghala:*  
   Kukamilisha utekelezaji wa mradi wa maghala, na kama kuna changamoto, ziwasilishwe Wizarani kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi.

 5.⁠ ⁠*Kujiendesha kwa Faida:*  
   Shirika linapaswa kujiendesha kwa faida na sio hasara. Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na wajumbe wa Bodi wanapaswa kuisimamia Menejimenti ya Shirika kuhakikisha miradi inayoibuliwa inakuwa na tija.

 6.⁠ ⁠*Utaalamu wa Bodi:*  
   Waziri Silaa amesema Bodi ina mchanganyiko wa taaluma, wakiwemo wataalamu wa mifumo, masuala ya Posta, na wakaguzi wa masuala ya fedha. Hatarajii kuona Posta ikifanya vibaya.

 7.⁠ ⁠*Ufuatiliaji wa Utekelezaji:*  
   Anatarajia kuona Bodi hii ikizunguka kuona hali halisi ya Shirika, na kutoa taarifa kuhusu ufanisi wa utekelezaji wa miradi kama Huduma Pamoja na duka la mtandao.

 8.⁠ ⁠*Kazi na Malalamiko:*  
   Waziri Silaa amesisitiza kuhusu kuwepo kwa kesi na malalamiko mbalimbali ndani ya Shirika, na kuelekeza Bodi kuhakikisha inashughulikia malalamiko hayo.

 9.⁠ ⁠*Mikopo:*  
   Kwa maeneo ambayo mnataka dhamana ya mali za Shirika kuchukua mikopo, taarifa inapaswa kuwasilishwa Wizarani kabla ya utekelezaji wa uchukuaji wa mikopo au uuzaji wa mali za Shirika.

10.⁠ ⁠*Umoja na Ushirikiano:*  
    Ili kuwa na mafanikio ndani ya Shirika, lazima kuwe na upendo, umoja, na kusikilizana kati ya Bodi, Menejimenti, na Watumishi. Watumishi wanapaswa kupewa nafasi ya kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ubunifu.

11.⁠ ⁠*Pongezi kwa Mafanikio ya Kimataifa:*  
    Waziri Silaa amewapongeza Shirika kwa kufanya vizuri kwenye maeneo ya kimataifa na kuwashauri kuwa mabalozi wazuri wa Shirika.

Waziri Silaa ameweka wazi kuwa kutekeleza maelekezo haya kutasaidia Shirika la Posta kuboresha huduma zake na kukidhi mahitaji ya wateja.