Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE ATEUA TUME YA KUTATHMINI UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nauye ametangaza tume ya watu tisa wakataofanya kazi ya Kutathimini hali ya uchumi katika vyombo vya habari nchini.

Waziri Nape ametangaza kamati hiyo leo tarehe 24 Januari 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alimuagiza kushughulikia suala la uchumi kwenye vyombo vya habari.

"Tumekua na majadiliano na tumefikia maamuzi ya kuunda timu ambayo itakwenda kufanya kazi ya kutathmini hali ya uchumi wa vyombo vya habari na wanahabari, na kuleta mapendekezo" Amesema Waziri Nape

Mhe Nape amesema kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wake atakuwa ni Mtendaji Mkuu Azam Media Group Ndg Tido Mhando huku katibu wa kamati hiyo akiwa ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg Gerson Msigwa.

Huku wajumbe wakiwa ni Bakari Machumu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji MCL, Joyce Mhavile Mkurugenzi Mtendaji ITV na Redio One, Dkt Rose Reuben Mkurugenzi Mkuu TAMWA, Keneth Simbaya Mkurugenzi Mtendaji UTPC, Sebastian Maganga Mkuu wa Maudhui Clouds Media, Jacqueline Woiso Mkurugenzi Mtendaji Multichoice Tanzania na Richard Mwaikenda Mwandishi wa kujitegemea.