Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE ASHIRIKI MKUTANO WA SHIRIKA LA MAWASILIANO LA JUMUIYA YA MADOLA


Mhe. Waziri Nape akizungumza katika Mkutano wa “Ministerial Alliance for Digital Nations” unaofanyika tarehe 21 – 22 Februari, 2023 Jijini London, Uingereza.

Mkutano huu umeandaliwa na Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (Commonwealth Telecommunications Organization’s – CTO). 

Lengo la msingi wa mkutano huu ni kuwaleta pamoja Mawaziri wote wanaohusika na Mawasiliano ya Simu na TEHAMA wa nchi za Jumuiya ya Madola ili kujadili masuala ya Maendeleo na Madiliko ya TEHAMA ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola. 

Mkutano huu pamoja na mambo mengine utaangalia changamoto zilizopo kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola katika kufikia lengo la maunganisho ya mtandao wa kasi kwa bei nafuu (challenges being faced in achieving the goal of affordable universal broadband connectivity) ikiwa ni kipengele muhimu cha mipango ya mabadiliko ya kidijiti.