Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE AMLILIA MAREHEMU KAPEMBE, AMPA TUZO YA KIHISTORIA


Na Juma Wange, WHMTH, KILIMANJARO

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amesema marehemu Joackim Kapembe aliweza kufika mapema katika kilele cha Mlima Kilimanjaro huku akiwa na vifaa vizito vya picha lakini aliweza kumsubiri na yeye afike ili aweze kuchukua pucha za tukio zima na yeye ndiye aliyemfanya apate nguvu pindi alipofika katika kilele hicho.

Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa Hafla ya Kukabidhi Vyeti, Tuzo na Zawadi kwa Waliofikisha Huduma ya Mawasiliano katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, leo Julai 22, 2023, Marangu Gate, Mkoani humo.

Marehemu Joackim kapembe alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na alifariki wakati wa kushuka mlima kilimanjaro wakati akiwa anawahisha taarifa za matukio aliyochukua wakati wa hafla ya kufikisha mawasiliano ya intaneti ya kasi katika kilele cha mlima huo tatehe 13 Disemba, 2022.