Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA MAREKANI


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Marekani ulioongozwa na Naibu Waziri wa Biashara za Kimataifa wa Marekani Bi. Maria Lago, leo  Februari 7, 2023 jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yamehusisha maeneo ya ushirikiano kati ya nchi Tanzania na Marekani kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipozungumza na Wafanyabiasha wa Marekani alipotembelea Nchi hiyo mwaka jana 2022.