Habari
WAZIRI NAPE AKUTANA NA MKURUGENZI MPYA WA USAID NCHINI TANZANIA

Na Jumaa Wange, WHMTH, Dodoma
Agosti 22, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi Mpya “Mission Director” wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Craig Hart ofisini kwake jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yalilenga zaidi mashirikiano katika kuboresha matumizi ya Teknolojia ili kuwezesha huduma nyingine zikiwemo Kilimo na Afya, mashirikiano katika kukuza Taasisi changa za Startup, mashirikiano katika kuwezesha miji ya kisasa (Smart City) pamoja na kutumia Teknolojia mpya ya 5G katika kuboresha uchumi wa Kidijitali.
Pia ziara hiyo ya Craig Hart ilikuwa ni kujitambusha kama Mkurugenzi Mkazi mpya wa Shirika la Kimarekani la USAID nchini Tanzania huku akichukua nafasi ya Bi. Kate Somvongsiri aliyemaliza muda wake.