Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE AKAGUA HUDUMA ZA MAWASILIANO MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb), leo Machi 15, 2024 ametembelea kijiji cha Kirongwe, wilaya ya Rorya, mkoani Mara na kukagua  huduma za mawasiliano katika eneo hilo.

Katika ziara hiyo, Waziri Nape alikagua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Halotel ambao umekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha huduma za mawasiliano katika eneo hilo la mpakani. 

Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Nape alitembelea Muhuru Bay mpakani mwa Tanzania na Kenya na kuzungumza na watendaji wa ofisi za uhamiaji upande wa Tanzania na Kenya.

Waziri Nape alielezea kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa huduma bora za mawasiliano katika maeneo ya mpakani, na mara kwa mara wananchi huko wamekuwa wakitumia huduma za mawasiliano za nchi jirani.

Waziri Nape ameliagiza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha inafikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika eneo la mpaka huo ili kuongeza nguvu ya mawasiliano katika eneo hilo la mpaka.

Jumla ya minara 758 inajengwa nchini kote ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini, ambapo kwa wilaya ya  Rorya imepata jumla ya minara 10.