Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, amekutana na ujumbe kutoka Benki ya Dunia na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali (Digital Tanzania Project).

 

Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilijadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo unaolenga kuimarisha miundombinu ya TEHAMA, kuongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali kwa wananchi, pamoja na kukuza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za umma na maendeleo ya uchumi wa kidijitali nchini.