Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA KAMPUNI CHANGA ZA TEHAMA, AJADILI FURSA NA CHANGAMOTO


Na Mwandishi Wetu – WMTH, Dar es Salaam.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), amekutana na wawakilishi wa Kampuni Changa (start-ups) zinazojishughulisha na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kujadili fursa zilizopo katika sekta hiyo pamoja na changamoto zinazowakabili katika kuanzisha na kukuza biashara zao nchini.

Katika kikao hicho, wawakilishi wa Start-ups hizo zimewasilisha uzoefu wao, fursa wanazoziona katika uchumi wa kidijitali pamoja na changamoto zinazohusiana na upatikanaji wa mitaji, masoko, miundombinu ya TEHAMA, ujuzi na mazingira ya biashara. 

Waziri Kairuki amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira yanayowezesha ubunifu na ukuaji wa Start-ups za TEHAMA, ili kuongeza ajira, kuchochea uwekezaji na kukuza uchumi wa kidijitali. Amesisitiza pia umuhimu wa Kampuni Changa kutumia fursa zinazotokana na teknolojia mpya na ubunifu katika kutatua changamoto za jamii na kuongeza ushindani wa Tanzania katika uchumi wa kidijitali.