Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI ATEMBELEA OFISI YA TCRA, ZANZIBAR


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed leo Agosti 1, 2022 ametembelea ofisi ya TCRA Zanzibar ikiwa ni mkakati wa kutembelea Taasisi za Muungano zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Mhe. Dkt Mohammed ameridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka hiyo ambayo kwa kushirikiana na Wizara anayoiongoza wamefanikiwa kutatua tatizo la mawasiliano katika maeneo mbalimbali Zanzibar.

Ameongeza kuwa kwa kushirikiana huko minara ya mawasiliano ipatayo 42 imejengwa katika maeneo yaliyokuwa hayana mawasiliano na maeneo yaliyokuwa na mawasiliano hafifu na tayari minara hiyo inafanya kazi.

Aidha, ametoa rai kwa watendaji na wananchi kutumia huduma za mawasiliano vizuri kwa kuzielekeza katika maeneo yenye tija kwa Taifa.

Naye Meneja wa TCRA Ofisi ya Zanzibar, Esuvatie Massinga amesema ugeni wa Waziri huyo katika ofisi za TCRA, zimeonesha ushirikiano na uhakika wa mashirikiano zaidi baina ya Mamlaka hiyo na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Dkt. Mohammed ameambatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo Dkt. Mzee Suleiman Mndewa  ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCRA na kupokelewa na  Meneja wa Ofisi ya TCRA Zanzibar Bi. Esuvatie Masinga pamoja na watumishi wa TCRA ofisi ya zanzibar.