Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

Serikali Yaahidi Mazingira Wezeshi kwa Watengeneza Maudhui Mtandaoni


Na Mwandishi Wetu, WMTH – Dodoma

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ili kuwawezesha wadau wa sekta ya sanaa kufanya kazi zao kwa ubora na tija.

Waziri Kairuki ameyasema hayo 
tarehe 14 Januari 2026, alipofanya mazungumzo na mtengeneza maudhui ya mtandaoni, Bw. Vicent Pendael Njau maarufu kama KIREDIO, aliyefika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, masuala yaliyojadiliwa ni pamoja upatikanaji wa huduma ya intaneti ya uhakika, fursa za kujipatia kipato kupitia mitandao ya kijamii, pamoja na uwepo wa sera na mifumo ya kiserikali ikiwemo ya kikodi inayogusa sekta ya ubunifu na maudhui ya mtandaoni.

Waziri Kairuki alimpongeza Bw. Njau (Kiredio) kwa kazi nzuri anayofanya na kutoa wito kwa  watengeneza maudhui pamoja na wasanii kwa ujumla kuzingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania pindi wanapotengeneza maudhui yao na kabla ya kuyaweka mtandaoni.

Kwa upande wake, Kiredio ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasikiliza vijana na kutambua mchango wao katika uchumi wa kidijitali, huku akiwasilisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya utengenezaji wa maudhui ili zifanyiwe kazi kwa wakati na kuiwezesha sekta hiyo kuendelea kukua.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mohammed Abdulla pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
na Teknolojia ya Habari.