Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WATUMISHI WA SEKTA YA MAWASILIANO WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA e-MREJESHO


Na Mwandishi Wetu - WMTH, Dodoma

 

Watumishi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wamepatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa e-Mrejesho yaliyotolewa na waratibu wakuu wa mfumo huo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 

Mafunzo hayo ya siku nne yameanza leo tarehe 09 Juni 2026, katika ofisi zilizopo Mji wa Serikali, Dodoma huku yakihusisha pia watumishi kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Tume ya TEHAMA (ICTC) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC).

 

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watumishi katika matumizi sahihi ya mfumo huo ili kuboresha upokeaji, ufuatiliaji na utatuzi wa kero, malalamiko, maoni na mapendekezo yanayotolewa na wananchi. Kupitia mfumo wa e-Mrejesho, taasisi za umma zinawezeshwa kutoa majibu kwa wakati na kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa wananchi.