Habari
WATENDAJI WA KATA JIJINI ARUSHA WAFANYA MAJARIBIO YA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI (NaPA)
Watendaji na wakusanya taarifa wa kata zilizopo Jiji la Arusha wamefanya majaribio ya matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi (NaPA) pamoja na kujifunza namna ya kuhuisha taarifa za watu na makazi kwa usahihi na ufanisi.
Zoezi hilo limefanyika leo, tarehe 10 Juni 2026, baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na wataalam kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Arusha iliyopo jijini Arusha.
Watendaji hao wamefanya majaribio hayo kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la kuhuisha taarifa za wakazi wa Kata ya Kati na Unga Limited, ambalo linatarajiwa kuanza rasmi kesho, tarehe 11 Juni 2026.
Zoezi hilo linalenga kuboresha usahihi wa taarifa za wakazi na makazi, pamoja na kuimarisha matumizi ya mfumo wa anuani za makazi katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kiutawala.
