Habari
WADAU TOENI MAONI CHANYA YA TEHAMA

Na Chedaiwe Msuya, WHMTH, Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia, Selestin Kakele amesema watu watoe maoni chanya katika matumizi ya TEHAMA ili kuboresha maisha ya watanzania katika ulimwengu wa kidigitali.
Hayo amebainisha leo Septemba 27 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu huyo wakati akifungua kikao cha kutoa maoni kuhusu ya sera ya Taifa ya TEHAMA kwaajili ya makundi Anuai amesema hichi wanachofanya wataendelea kwa makundi mengine.
Amesema wizara zote ni kutunga na kusimamia sera, kanuni, miongozo na sheria ambayo huwa inasimamia utekelezaji wa majukumu wizara wanatekeleza wajibu wa msingi.
"Sera ya TEHAMA ya mwaka 2016 ni mda mrefu umepita na TEHAMA na kama kiumbe ambacho kinazaliwa kinakua na kinabadilika kulingana na wakati na mambo mbalimbali yanatokea duniani katika jamii,"amesema Kakele.
Amesema wakati wanatunga sera hiyo mwaka 2016 hakukuwa na mambo ambayo leo yanatokea hatakama yalikuwepo hakuana mtu angeweza kufasihi miaka michache ambacho kinatokea leo ingekua je?.
Amesema Teknolojia inakua kwa kasi sana ipo haja ya kufanya marejeo ya sera ya TEHAMA zipo taratibu za kuandaa sera moja ya shariti la msingi ni ushirikwishaji wa jamii.
"Tumekuwa na utaratibu huu tangu tunaanza mchakato wa kukutana na makundi mbalimbali na leo tumeona tukutane na makundi Anuai wenye changamoto mbalimbali za ulemavu lakini ni wadau wetu muhimu katika sera tunajaribu kuifanyia mapitio,"amesema.
Aidha amesema wanataka sera hiyo watakuwa wamekubaliana na kukamilika itumike kujibu changamoto na kuwasaidia kutoa majawabu changamoto zinazowakabili watu kwenye makundi anuai katika mlengo wa TEHAMA.
Ameongeza kuwa watawezeshaje taasisi za serikali na sekta binafsi zinakihusisha na TEHAMA kuzingatia mahitaji maalumu katika utoaji huduma zao.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Watu Wenye Ulemavu Nchini(SHIVAWATA), Ernest Kimaya amesema sera ya TEHAMA ni muhimu kwa watu wenye ulemavu kutoa maoni kuboresha sera.
Naye Afisa Habari Chama cha Wachimbaji Wanawake Madini, Halima Mhando amesema hakuna maendeleo yeyote bila mawasiliano kwa sasa hakuna kitu kinafanyika bila TEHAMA watatoa maoni yenye tija.
Kikao hicho kiliweza kuhudhuriwa na Bw. Mohamed Mashaka Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Mifumo na Huduma za TEHAMA (DISDS), Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali,Bw.Baraka pamoja na baadhi wa viongozi wa Wizara.