Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

UJUMBE WA TANZANIA WATEMBELEA KAMPUNI ZA SATELITE BEIJING, CHINA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla akiwa na ujumbe wa wataalam kutoka Tanzania wamepotembelea Kampuni ya  Satelaiti ya China (China Satcom) inayojishughulisha na utoaji wa huduma za Mawasiliano kupitia Satelaiti leo Mei 29, 2024 Beijing, China

 

Na Mwandishi Wetu,WHMTH

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla ameongoza ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wataalamu wa mawasiliano kuzuru Kampuni za Satelite za China SATCOM na Space Star Technology Ltd. zilizopo Beijing, China.

Ziara hiyo iliyofanyika leo Mei 29, 2024 ilikuwa na lengo la kujifunza na kupata uzoefu kuhusu teknolojia ya anga na utoaji wa huduma za mawasiliano kwa njia ya Satelaiti 

Pamoja na ziara hiyo wataalamu wa Tanzania na China wamefanya kikao cha majadiliano na kubadilishana ujuzi kuhusu teknolojia hiyo muhimu ikiwa ni muendelezo wa ziara ya mafunzo kwa wataalam kutoka Tanzania kuhusu uendeshaji wa Satelaiti yaliyoanza Mei 27, 2024.

Katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepanga kuanza utekelezaji wa kuunda na kurusha Satelaiti yake angani kwa lengo la kurahisisha matumizi ya teknolojia ya anga inayochochea mapinduzi ya kidijiti.

Aidha, mpaka sasa Tanzania imeshapata obiti mpya ya setelaiti ya 16 degrees West kwa matumizi ya Satelaiti za Utangazaji na masafa mapya yatakayotumika katika kuboresha usalama wa mawasiliano ya angani na majini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla akiwa katika majadiliano na Wataalam wa Kampuni ya  Satelaiti ya China (China Satcom) iliyopo Beijing, China leo tarehe 29 Mei, 2024.

Matukio katika picha ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla akiwakiongoza timu ya wataalam wa masuala ya Mawasiliano kutoka Tanzania kwenye ziara ya kutembelea Kampuni inayojishughulisha na Teknolojia ya Anga (Space Star Technology Ltd.) iliyopo katika kituo cha Satelaiti cha Yu