Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

UHURU WA MTANDAO ZINAPASWA KULINDA TAMADUNI ZA NCHI-WAZIRI NAPE


Na Chedaiwe Msuya, WHMTH, Dar es Salaam.

Waziri wa Habari,Mawasilino na Teknolojia, Mhe.Nape Nnauye (Mb) amesema nchi itaendelea kuwa waumini wa uhuru wa mtandaoni huku akitoa rai kuwa uhuru huo unapaswa utumike kulinda tamaduni za Bara Afrika. 

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 28 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Jukwaa la uhuru wa mitandao barani Afrika 
Uliofanyika jijini Dar es salaam uliohudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka nchi tofauti.

Amesema  nchi kutoa uhuru wananchi wanapaswa kulinda tamaduni kwa kutumia mitandao hiyo katika shughuli za kuwaingizia kipato na si kutumia katika mambo ambayo yanaweza kuvunja amani ya nchi.

"Tumeweka katika sera zetu uhuru wa mitandao lakini sasa hivi dunia imekuwa digital tumieni mitandao hiyo kufanya shughuli za kiuchumi na si kupiga umbea ambao haukusaidii chochote na mitandao ni fursa, "amesema Nape.

Amesema pamoja na kuwa na uhuru mtandaoni nchi za Afrika zinapaswa kulinda tamaduni na ili kuepusha nchi hizo kuingia kwenye matatizo ambayo yatapelekea kuharaibu Amani na kuleta machafuko.

"Tusiondoke kwenye mtandao kila mtu ajiunge huko lakini tuhakikishe tunabaki salama kwa maslahi ya nchi zetu na kubadilisha maisha yetu kwa kufanyabiashara," amesema. 

Waziri Nape amesema kuwa nchi inajipanga chaguzi zijazo ziweze kutumia teknolojia kwenye uchaguzi ili kumuezesha kila mtu kuchagua viongozi popote atakapokua.

"Tunataka ifike mahali kila mwananchi awe na uwezo wa kupiga kura mtandaoni kusiwe na haja ya kwenda kwenye vituo na kupanga foleni kama kila mtu anaweza kutumia simu basi inawezekana ni sisi kuamua kwa kuweka sera nzuri na utekelezaji"ameongeza Nape

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Neema lungangila amesema kuwepo kwa mkutano huo nchini kumetoka na juhudi zinazofanywa na Rais Dk  Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi kimataifa na kuimalisha uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.