Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TUZO ZATOLEWA KWA WALIOFIKISHA MAWASILIANO KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO


Na Juma Wange, WHMTH, KILIMANJARO

Itakumbukukwa mwaka jana Tarehe 13 Disemba, 2022, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye aliongoza Viongozi mbalimbali wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), HUAWEI, Watumishi wa Wizara hiyo na wadau mbalimbali katika kufikisha Intaneti yenye kasi katika kilele cha Mlima mrefu barani Afrika Mlima Kilimanjaro.

Aidha, leo Julai 22, 2023 Mhe. Nape Nnauye amegawa na kupokea Tuzo maalumu kwa Waliofikisha Huduma ya Mawasiliano katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, Marangu Gate, Mkoani Kilimanjaro.

Kati ya waliopewa tuzo hizo ni Marehemu Joackim kapembe ambapo tuzo hiyo ilipokelewa na mkewe.

Vilevile Mhe. Nape ameongoza hafla hiyo katika kumkumbuka marehemu Kapembe aliyefarika kwa ajali wakati akishuka mlima huo mara baada ya kufanikisha zoezi la kupeleka mawasiliano ya Intaneti katika mlima huo.