Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TUWAPENDE NA KUWAHESHIMU WASAIDIZI WA VIONGOZI, MADEREVA - DKT.YONAZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa kuna haja ya kuwaheshimu na kuwapenda wasaidizi wa viongozi wakiwemo wasaidizi wa ofisi, madereva na makatibu mukhtasi kwa kazi ngumu wanazofanya kuwasaidia viongozi kutekeleza wajibu wao kwa taifa.

Dkt. Yonazi ameyasema hayo wakati wakati wa kuhitimisha kikao cha tathmini ya utendaji kwa Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake leo tarehe 29,Julai 2022 jijini Arusha.

“Thamani ya Watumishi hawa imejengwa katika utu wao, unaochangia katika maendeleo ya nchi yetu. Tuwaheshimu na kuwapenda,” amesema Dkt. Yonazi.

Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na zile zaTaasisi zake zote, wamekuwa na Kikao kazi (Retreat) cha kufanya tathmini ya utendaji wa kazi zake na kujipanga katika kutekeleza bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023. Mada mbaalimbali ziliwasilishwa katika Kikao hicho ikiwemo Uongozi na Utawala Bora iliyotolewa na Taasisi ya Uongozi, Protokali na Ustaarabu, Mbinu mbalimbali za Mawasiliano ya Kimkakati na Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali.