Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA WSIS, USWISI


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) , akiongozana na Naibu Katibu Mkuu , Bw. Nicholaus Mkapa ameongoza  kikao kazi cha ujumbe wa Tanzania katika ofisi ya balozi na mwakilishi wa wakudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kabla ya Mkutano wa Dunia wa Jumuiya ya Habari (WSIS) kwa mwaka 2024 (WSIS 2024). 

Mkutano huu unalengo la kujadili  masuala mbalimbali ya TEHAMA na uwezo wake katika kukuza maendeleo, kuimarisha upatikanaji wa habari na maarifa, kuchochea ustadi na kuhamasisha matumizi ya TEHAMA kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi..Mkutano huu unafanyika jijini Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 27 hadi 31 Mei 2024.

Ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huu ni moja ya jitihada katika kuimarisha mashirikiano yake duniani katika kukabili changamoto mbalimbali katika TEHAMA na kuongeza tija katika utekelezaji wa miradi ya TEHAMA.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.), pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholaus Mkapa wamepokelewa na Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mara baada ya kuwasili nchini Uswisi ambapo atashiriki Mkutano wa Dunia wa Jumuiya ya Habari (WSIS) kwa mwaka 2024 (WSIS 2024).