Habari
Tanzania Yashiriki Mjadala wa Ngazi ya Mawaziri katika Jukwaa la WSIS Geneva
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), ameshiriki Mjadala wa Ngazi ya Mawaziri (Ministers' Round Table) uliofanyika katika Kongamano la Kimataifa kuhusu Jamii ya Habari (World Summit on the Information Society - WSIS) 2026 tarehe 09 Julai, 2026 jijini Geneva, Uswisi.

Ushiriki wa Tanzania katika mjadala huo umeendelea kuonesha dhamira ya nchi ya kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuharakisha mageuzi ya kidijitali, kukuza matumizi salama na jumuishi ya teknolojia pamoja na kuhakikisha maendeleo ya kidijitali yanawanufaisha wananchi wote.
