Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TANZANIA YAONESHA DIRA YA KIDIJITALI DUNIANI


•⁠  ⁠Yatoa Tamko la Kushiriki Uchaguzi wa Nafasi za Uongozi UPU

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry William Silaa ametoa tamko rasmi la Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 28 wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) unaoendelea Dubai.

Tamko hilo alilolitoa kwa njia ya mtandao, Waziri Silaa ameeleza kuwa, Serikali ya Tanzania kupitia Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali 2024–2034, imejipanga kuunganisha teknolojia za kidijitali katika sekta zote, kuboresha huduma za posta, kukuza biashara mtandaoni na kuimarisha ujumuishi wa kifedha kwa wananchi.

Waziri Silaa amesema kuwa, Tanzania iko tayari kuongoza mageuzi ya kidijitali barani Afrika na duniani, kwa huduma bora, jumuishi na shindani kimataifa.

Katika tamko hilo, Tanzania imetangaza pia dhamira ya kuendelea kushiriki kikamilifu UPU na kuwania tena nafasi za uongozi katika Baraza la Uendeshaji (POC) na Baraza la Utawala (CA) kwa kipindi cha 2026–2029.