Habari
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Ushiriki wa Kimataifa katika Usimamizi wa Akili Unde (AI)
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), ameshiriki katika hitimisho la Global Dialogue on AI Governance lililofanyika Geneva, Uswisi, likihitimisha majadiliano ya ngazi ya juu yaliyowakutanisha viongozi, watunga sera na wadau wa teknolojia kutoka mataifa mbalimbali.
Ushiriki wa Tanzania katika jukwaa hilo unaonesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo na usimamizi wa Akili Unde (AI), ili kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika kwa uwajibikaji, usalama na manufaa ya maendeleo jumuishi.
Tanzania inaendelea kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kimataifa ili kuhakikisha inakuwa sehemu ya maamuzi yanayounda mustakabali wa uchumi na jamii ya kidijitali duniani.
#Tanzania #AI #AIGovernance #DigitalTransformation #Geneva
