Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TANZANIA YACHAGULIWA BARAZA LA UMOJA WA MAWASILIANO AFRIKA (ATU)


ALGERIA

Tanzania imechaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Umoja wa Mawasiliano Afrika (African Telecommunications Union - ATU) kwa kipindi cha miaka 4 (2023-2026).

Tanzania ni miongoni mwa nchi 25 zilizochaguliwa kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mawasiliano Afrika (ATU) 49.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliongoza kampeni ya Tanzania kuomba nchi wanachama wa ATU kuichagua Tanzania katika uchaguzi uliofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa sita wa Umoja huo (Conference of Plenipotentiaries) unaofanyika Jijini Algiers, Algeria.

Akichangia hoja katika Mkutano huo leo, Mheshimiwa Nape Alisisitiza juu ya umuhimu wa nchi za Afrika kujipanga kimkakati hususan katika chaguzi zinazofanyika katika mashirika ya Mawasiliano ya Kimataifa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU - International Telecommunications Union).