Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

SERIKALI YAUNGA MKONO KIKAMILIFU SEKTA BINAFSI NA MFUMO WA TEKNOLOJIA YA UVUMBUZI KUFIKIA MALENGO YA SDG


DAR ES SALAAM

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nauye amesema Serikali kupitia Wizara ya Habari inaunga mkono kikamilifu sekta binafsi na mfumo wa teknolojia ya uvumbuzi zinaongezwa katika kutoa suluhisho na kusaidia nchi kufikia malengo yake ya SDG.

Waziri ameyasema hayo Septemba 1 2022 katika ukumbi wa mikutano Mlimani City jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa serikali inapongeza maendeleo haya yaliyozinduliwa rasmi kibiashara hapa nchini na Upatikanaji wa mtandao wa kasi unaojulikana kama “Wireless ya Fibre” na kuipongeza Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuongoza katika ubunifu wa huduma na Teknolojia hapa nchini.

Amesema teknolojia hii itakuwa na manufaa katika sekta zote za uchumi na kijamii nchini na itasaidia kuleta maendeleo na mageuzi kwa watanzania wote na kupelekea Tanzania kuwa na uchumi wa Kidigiti.

“Teknolojia hii mtambuka, itanufaisha sekta zingine kama vile: Nishati, Madini, Ujenzi wa viwanda, Kilimo, Afya, Elimu na Usafiri. Lakini pia kuongeza kasi zaidi ya huduma za serikali mtandao. 

Haya yote, yakiwa ni maeneo ambayo serikali ya awamu ya sita imeyapa kipaumbele sambamba na Tanzania ya Kidijitali ambayo yote yanatiliwa mkazo na nia yetu ya kuboresha maisha ya watu wetu na kutengeneza fursa za ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla” ameyazungumza Waziri Nape

Amesema, mapema mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alithibitisha tena dhamira ya serikali ya kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini Tanzania na Serikali inathamini jukumu la sekta binafsi katika kukuza biashara na uwekezaji na itadumisha mazungumzo ya wazi ili kujenga na kuimarisha ushirikiano na makubaliano.

Amesema Serikali imekuwa ikiweka nguvu zake katika miradi na mipango kadhaa kueneza mawasiliano nchini ikiwemo upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Mradi wa Tanzania ya Kidijitali pamoja na Mradi wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.

“Tunafurahi sana kuona makampuni binafsi ikiwemo Vodacom yakiweza kutumia fursa na rasilimali hizi katika kuziongeza thamani. 

Teknolijia hii ya 5G ni njia moja itakayoongeza ufanisi wa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano kwa kuwezesha watumiaji wake kufikia kasi ambazo ni mojawapo ya malengo makuu ya serikali katika uwekezaji mkubwa katika mkongo huo, uzinduzi huu ni sehemu ya kutumiza ndoto zetu” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mawasilino na Teknolojia wa Kampuni ya Vodacom amesema, katika kuhakikisha maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania, watahakikisha mpaka kufikia mwaka 2024, watafikia asimia 90 ya watanzania kwa kushirikiana na serikali ya jamhuri ya muunganoi wa tanzania.