Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NaPA na HESLB Waanza Kutoa Elimu ya Maombi ya Mikopo Kagera


Timu ya wataalam wa Anwani za Makazi chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanza kutoa elimu kwa waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.

 

Zoezi hilo limeanza tarehe 25 Mei, 2026 katika eneo la Soko Kuu la Machinjioni, likiwa na lengo la kuwasaidia wanafunzi na wazazi kupata uelewa wa kina kuhusu taratibu za maombi ya mikopo pamoja na matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali wakati wa kufanya maombi hayo.

 

Programu hiyo itaendelea hadi tarehe 29 Mei, 2026 ambapo wananchi watapata nafasi ya kuuliza maswali, kupata msaada wa moja kwa moja kutoka kwa wataalamu pamoja na kuelekezwa namna bora ya kujaza taarifa muhimu zinazohitajika katika maombi ya mikopo.

 

Kupitia elimu hiyo, waombaji wanatarajiwa kuongeza uelewa kuhusu vigezo vya kupata mikopo na kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa kufanya maombi ya elimu ya juu.