Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU WAZIRI MKAMA ATETA NA MKUU WA MKOA WA KATAVI.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Switbert Zakaria Mkama, amtembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, kabla ya kuendelea na ziara ya kutembelea Miundombinu ya TEHAMA.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano, hususan upatikanaji na uboreshaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi.

Mhe. Dkt. Mkama amesisitiza umuhimu wa Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya mawasiliano katika kuhakikisha maeneo yenye changamoto za mawasiliano yanapatiwa ufumbuzi na wananchi wanapata huduma bora, za uhakika zinazopatikana kwa wakati. 

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kufuatilia utekelezaji wa miradi ya mawasiliano na kuhakikisha uwekezaji katika Miundombinu ya TEHAMA unaleta manufaa kwa wananchi.