Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

Naibu Waziri Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb.),  amekabidhi vishikwambi 101 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb.), 
amekabidhi vishikwambi 101 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza, Bw. Vincent Augustine Mbua, katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika tarehe 25 Februari, 2026, Naibu Waziri Dkt. Mkama amepongeza jitihada za Halmashauri ya Ukerewe kwa kuendelea kushirikiana na Wizara katika utekelezaji wa mikakati ya kidijitali, akibainisha kuwa matumizi ya teknolojia ni nguzo muhimu katika kuboresha maisha ya wananchi na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

Vishikwambi hivyo vinalenga kuchochea matumizi ya teknolojia ya kidijitali kwa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Ukerewe, pamoja na kuimarisha matumizi ya Mfuko wa Anwani za Makazi na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Serikali kwa njia ya kidijitali. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kuharakisha mabadiliko ya kidijitali nchini na kujenga mazingira bora ya utoaji huduma kwa wananchi kwa kutumia teknolojia.