Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AKAGUA HUDUMA ZA MAWASILIANO UNGUJA


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb.) amezuru katika Mkoa wa Kaskazini ‘A’ na Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kwa ajili ya kukagua upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo yaliyozungumziwa na waheshimiwa wabunge kuwa na changamoto ya Mawasiliano.

Kabla ya kuanza ziara hiyo Novemba 22, 2024, Mhe. Mahundi alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Khalid Salumu Mohammed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi  wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mahundi amekagua hali ya mawasiliano Unguja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano wa Honora inayojengwa katika maeneo ya Kibuteni na  Kisakasaka pamoja na kutembelea redio jamii ya Tumbatu FM.