Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU WAZIRI DKT. MKAMA AWASILISHA TAARIFA YA NIDC KWA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb), amewasilisha taarifa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma tarehe 13 Mei 2026.

 

Kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Ally Hassan Omar King (Mb), ambapo wajumbe walijadili na kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu Taarifa ya Utendaji wa Kituo cha Kuhifadhia Data cha Taifa (NIDC).

 

Akizungumza baada ya michango ya wajumbe wa kamati hiyo, Dkt. Mkama aliishukuru Kamati kwa ushauri walioutoa na kubainisha kuwa Serikali itaendelea kuufanyia kazi ili kuimarisha utendaji na maendeleo ya sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini.