Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI ATEMBELEA TAASISI ZA MAWASILIANO - ZANZIBAR


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla katika kukamilisha ziara yake mjini Zanzibar ametembelea ofisi za Taasisi za Muungano zilizo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), tarehe 30 Agosti, 2022.
 
Aidha katika nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bw. Abdulla alipata wasaa wa kufanya kikao cha pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi hizo lengo ikiwa ni kupata taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo, mjini humo
 
Sambamba na hilo, Bw. Mohammed Abdulla ameongeza kuwa, lengo si tu kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo bali pia kuona namna Taasisi za sekta ya Mawasiliano nchini zinashiriki kikamilifu katika kuipekea Tanzania kwenye uchumi wa kidijitali.
 
Katika ziara hiyo Bw. Mohammed Abdulla aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bi. Caroline Kanuti Pamoja na maafisa mawasiliano wa Wizara hiyo.