Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU KATIBU MKUU WHMTH AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA UMOJA WA ULAYA


Na Juma Wange

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (EU) leo tarehe 22 Juni, 2022 jijini Dodoma ulioongozwa na Mkuu wa Ushirikiano wa umoja huo Cedric Mellel.

Kikao kazi hicho kimejadili utekelezaji wa mradi wa DIGITAL4TANZANIA wenye jukumu la kuboresha mawasiliano katika maeneo ya vijijini, kuboresha sheria kuhusu kuunda taarifa binafsi (Data Protection) kwa ajili ya kulinda taarifa hizo.

Mradi huo wenye thamani ya Bilioni 85 ambao utatekelezwa katika kipindi cha miaka minne pia utasaidia kuunganisha taasisi za serikali katika mtandao wa Pamoja na kuongeza huduma mbalimbali za wananchi ambao hawana huduma hizo.

Kikao kazi hicho pia kimejadili umuhimu wa kuboresha Mawasiliano maeneo ya vijijini, kusaidia makundi mbalimbali ikiwemo ya wanawake katika sekta ya ujasiriamali.