Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

NAIBU KATIBU MKUU ATEMBELEA UCSAF


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla leo Agosti 10, 2022 ametembelea Makao Makuu ya Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) zilizopo jijini Dodoma.

 Pamoja na mambo mengine Naibu Katibu Mkuu Abdulla amefanya kikao cha pamoja na wafanyakazi wa Mfuko huo kwa lengo la kupata taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko.

 Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo akiambatana na Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Bi. Justina Mashiba ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya za UCSAF unaoendelea katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 97.