Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MKONGO WA MAWASILIANO KUPANDA MLIMA KILIMANJARO


 

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limekaribia kumaliza kuufikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika kilele cha  Mlima Kilimanjaro.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Peter Ulanga  Julai 30, 2022,  alipotembelea timu ya wataalamu wa TTCL walioko kwenye kazi ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Mlima Kilimanjaro katika kituo cha Horombo ambacho kipo Mita 3720 juu ya usawa wa bahari.  

Ufikishaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika kilele cha Mlima Kilimanjaro utawezesha upatikanaji wa  huduma za mawasiliano katika Mlima huo na kuvutia zaidi watalii sambamba na kuongeza usalama wa watalii na waongoza watalii na kuliongezea Shirika la Mawasiliano Tanzania vyanzo vya Mapato.  

Kazi ya kufikisha Mawasiliano mpaka kituo cha Kibo Hut (Basecamp) inatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwezi Agosti 2022.