Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MIFUMO YA HOSPITALI KUUNGANISHWA: WAZIRI NAPE


Na WHMTH, Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa hospitali zimekuwa na mifumo mingi na haisomani kiasi ambacho imechangia kuongezeka kwa gharama za matibabu kwa wananchi.

Waziri Nape ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya tatu ya kidijitali ya Afya na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili katika kampasi ya Mloganzanziala, jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya kufunga mafunzo hayo Waziri Nape amesema maonesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi ili kujadili namna TEHAMA inavyoweza kuboresha huduma za Afya.
 
“Tunataka kwa kupitia TEHAMA tuboreshe huduma hiyo ili mtu akienda kokote taarifa zake ziwepo,” amesema Waziri Nape.
 
Waziri Nape ameeleza jitihada mbalimbali zinazofanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kufanya mifumo ya TEHAMA isomane ili kuweza kupunguza gharama kubwa ya matibabu kwa wananchi Pamoja na zile za uendeshaji.
 
Pa Waziri Nape amesema Kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye mkongo wa Taifa wa mawasiliano ambao ndo njia kuu ya kupeleka hizo taarifa na kuna mifumo kadhaa lazima itengenezwe ili taarifa ziwe pekee kwa kila mtu.